February 6, 2021

 


INAAMINIKA kwamba nyota wa kikosi cha RB Leipzig,  Dayot Upamecano ni miongoni mwa orodha ya majina yaliyopo kwenye mpango wa Kocha Mkuu wa Chelsea,  Thomas Tuchel. 

Ripoti zinaeleza kuwa Tuchel ambaye ni mrithi wa mikoba ya Frank Lampard macho yake kwa upande wa usajili yanatazama nyota ambao wanashiriki Bundesliga na anahitaji beki wa kati.

Tuchel tayari ameanza kazi ndani ya Stamford Bridge huku akionekana kuleta mabadiliko ndani ya timu na ana matumaini ya kuboresha zaidi kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao.

Kwa mujibu wa Bild,gazeti la habari la Ujerumani limeripoti kuwa Tuchel katika akili yake kuna majina ya mabeki watatu ambao ni Niklas Sule na David Alaba wa Bayern Munich pamoja na Upamecano.

Alaba mwenye miaka 28 pia anatajwa kuwaniwa na Liverpool pamoja na Liverpool ambao nao wanawania saini yake.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic