MASHABIKI wa Yanga ambao ni vinara wa Ligi Kuu Bara leo watakuwa na fursa ya kumuona nyota wao mpya, Fiston Abdol Razack kwa kiwango cha buku tatu tu pamoja na mastaa wao wengine ambao ni Deus Kaseke, Michael Sarpong, Metacha Mnata.
Yanga ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ipo nafasi ya kwanza na imekusanya jumla ya pointi 44 baada ya kucheza mechi 18 ndani ya ligi ikiwa haijapoteza zaidi ya kulazimisha sare tano na kushinda mechi 13.
Leo itakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya African Sports ya Tanga, inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Uwanja wa Azam Complex ukiwa ni mchezo wa kujipima nguvu.
Ofisa Uhamasishaji wa Klabu ya Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kiingilio jukwaa kuu itakuwa 5,000 na mzunguko itakuwa ni 3,000, lengo ni kuonyesha upana wa kikosi cha Yanga kuelekea kwenye mzunguko wa pili.
Ni bora mngejipima kwa timu yenye kiwango ili mjuwe kiwango chenu cha uhakika
ReplyDeleteVipi matokeo mbona hatujulishwi?
ReplyDelete