February 4, 2021

 


KOCHA mkuu wa klabu ya AS Vita ya nchini Congo amefunguka kuwa mchezo wao wa kwanza wa  Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Simba utakuwa mgumu, kutokana na timu hiyo kupata mechi nyingi za kirafiki ambazo anaamini.

AS Vita na Simba katika ligi ya mabingwa zote zipo kundi A ambapo zinatarajia kumenyana katika mchezo wa kwanza kwa timu zote katika kundi hilo ambapo AS Vita inatarajia kuwa mwenyeji wa Simba katika mchezo utakaofanyika Februari 12 mwaka huu nchini Congo.

Ibenge amesema kuwa mechi za kirafiki za Simba ilizocheza dhidi Al Hilal na TP Mazembe ni maandalizi mazuri kuelekea mchezo wao ambao anaamini utakuwa mgumu kutokana na ubora wa timu zote hizo mbili.

“Simba wamejiandaa vizuri kuelekea mchezo dhidi yetu, kucheza dhidi ya Al Hilal na TP Mazembe kisha wakapata matokeo basi inaonyesha ni kwa kiasi gani kuwa wanatimu nzuri na wana malengo mazuri na michuano hii.

“kwa upande wetu ushindi ni jambo la muhimu kwa kuwa tutakuwa nyumbani sehemu ambayo ni muhimu kwetu kuibuka washindi, najua haitakuwa rahisi kwa kuwa ukiitazama Simba utaona kuwa ni timu nzuri lakini tutafanya kila liwezekanalo kuwa washindi,” amesema kocha huyo.

3 COMMENTS:

  1. Simba nichombo kingine BWANA, hao wapinzani wetu kichapo tu hatuchezi na majina yao

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic