February 24, 2021

JAMHURI Kihwelo, 'Julio' Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes amesema kuwa kilichosababisha timu hiyo isipate matokeo ni ugeni katika mashindano hayo.

Ngorongoro Heroes ilikuwa inashiriki michuano ya Mataifa Afrika, (Afcon) hatua ya makundi ikiwa kundi C pamoja na timu za Ghana, Gambia na Morocco. 

Katika kundi hilo Tanzania imeambulia pointi moja baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Gambia.

Ilipoteza kwa kufungwa mabao 4-0  dhidi ya Ghana na mbele ya Morroco iliambulia kichapo cha mabao 3-0.

Julio amesema:"Ugeni wa mashindano kwenye kundi letu umetufanya tushindwe kupata matokeo tofauati na wengine ambao tulikuwa nao kwenye kundi.

"Tunamshukuru Mungu tumeshiriki salama ila ushiriki wetu pia kuna kitu ambacho tumejifunza hivyo itakuwa ni safari yetu ya mafanikio kwenye mashindano mengine,".

4 COMMENTS:

  1. Mpaka leo nimeshindwa kuelewa team yetu ilienda kufanya nn?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kupata uzoefu wa mashindano kama Julio alivyosema!!!

      Delete
    2. Haahaaa....nachekaaaaa...kila mashindano tunayoshiriki ni kujifunza na kupata uzoefu....hebu tutoleeni sababu zenu za pumba na msitufanye mafala.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic