February 7, 2021

 


PATRICK Aussems raia wa Ubelgiji yupo Kenya kwa ajili ya kumalizana na Klabu ya AFC Leopards ili akabidhiwe mikoba ya kuinoa timu hiyo.


Aussems ambaye alipewa jina la Uchebe na mashabiki wa Klabu ya Simba aliweza kuiongoza kikosi hicho kwa mafanikio msimu wa 2018.

Msimu huo aliweza kuipeleka Simba hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ila alishindwa kutinga hatua ya nusu fainali.


Mkataba wake ndani ya kikosi cha Simba ulisitishwa naomi wa 2019/20 kwa kile kilichoelezwa kuwa  ni mwendo mbaya ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na zile za Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo waliishia hatua ya awali.


Mikoba yake alimuachia Sven Vandenbroeck ambaye msimu huo aliweza kutwaa taji la Ligi Kuu Bara,  Kombe la Shirikisho na Ngao ya Jamii.


Msimu wake wa pili wa 2020/21 alibwaga manyanga na kuibukia ndani ya Klabu ya FAR Rabat ya Morroco ambapo huko ni Kocha Mkuu. 



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic