IKIWA leo Simba itashuka Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Azam FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kuna hatihati itawakosa nyota wake wanne.
Mchezo wa leo ni kiporo ambapo awali ilipangwa kuchezwa saa 1:00 ila Februari 6 taarifa rasmi kutoka Bodi ya Ligi Tanzania iliweka wazi kuwa mechi hiyo itachezwa saa 10:00 jioni.
Hawa hapa nyota wa Simba wanaotarajiwa kuukosa mchezo wa leo, Uwanja wa Mkapa ambao ni:-
Nahodha John Bocco yeye anasumbuliwa na majeruhi ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, dhidi ya FC Platinum.
Erasto Nyoni beki mkongwe ndani ya Simba naye pia hayupo fiti kutokana na kusumbuliwa na majeraha.
Ibrahim Ame, beki huyu wa kati bado hajawa fiti baada ya kupata majeraha na timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars.
Jonas Mkude, kiungo huyu alikuwa nje ya uwanja kwa muda kutokana.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa mchezo wa leo na watapambana kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.
0 COMMENTS:
Post a Comment