February 25, 2021


 KAMPUNI ya Afrisoccer kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Kampuni ya La Liga kutoka Hispania, imeandaa kongamano la soka huku aliyekuwa Kocha Mkuu wa Simba, Mbelgiji Sven Vandenbroeck akiwa mmoja wa watoa mada.

Kongamano hilo limepangwa kufanyika kati ya Machi 18 na 19, mwaka huu litakalofanyika kwenye Ukumbi wa Maktaba wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mratibu wa Kongamano hilo, Peter Simon, amesema kuwa wadau mbalimbali watashiriki mkutano wenye malengo ya kukuza na kuendelesha soka hapa nchini.

 

Simon aliwataja walengwa wa Kongamano hilo ni wadau wa soka ambao ni Serikali, Kamati za Michezo za Mikoa na Wilaya, TFF, Bodi ya Ligi Kuu Bara, klabu, Makocha na Mawakala wa Wachezaji.


Aidha aliwataja baadhi ya watoa mada katika Kongamano hilo ni Mlamu Mng’ambi (Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba), Senzo Mazingisa (Mshauri wa Yanga), Injinia Hersi Saidi (Makamu Mwenyekiti wa Usajili na Mashindano wa Yanga) na Martin Hamells (Wakala kutoka Ujerumani).

 

“Jumla mada sita zitakazowasilishwa katika Kongamano hili ambazo ni Masoko na Udhamini, Maendeleo ya soka la Vijana na Wanawake, Usimamizi wa Viwanja, Huduma za Uwakala, Vyanzo vya Mapato na Masuala ya Fedha kwa Klabu na Maendeleo ya Tehama na Soka.

 

“Tunaamini baada ya Kongamano hili baadhi ya klabu zitakuwa zimejifunza baadhi ya vitu na hasa jinsi ya uendeleshaji wa klabu, kwani lengo ni kuhakikisha soka linapiga hatua hapa nchini,” amesema Simon.

5 COMMENTS:

  1. Haji Manara anastahili kuwa mmoja wa watoa mada lakini sijui kwa nini hajajumuishwa!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Haji Manara atatoa mada gani ya maana mbele ya watu wenye akili zao!!!!!!,au unafikiri wanataka kusikia upuuzi wa yanga na simba?

      Delete
    2. Hahahahaha!!! Kaka usimdharau mtu kwa wajihi wake au kwa porojo anazozitoa katika hali ya utani wa Simba na Yanga huwezi jua ana kitu gani cha ziada kichwani mwake nje ya U Simba wake na mabezo yake kwa Yanga.
      Kuna watu wangapi wenye elimu zao za kutosha katika Simba na Yanga lakini wameshindwa kuleta mabadiliko chanya katika hizo timu

      Delete
  2. Ni jambo jema, lakini bado ajili zetu zimegandia Simba na Yanga. Kama tunataka kupata kitu kipya tungepata watoa Mara nje ya Simba na Yanga.

    ReplyDelete
  3. Good Idea, tutajifunza kitu kikubwa sana kutoka kwa watoa Mada. Kama yakifanyiwa kazi tunaweza kupiga hatua kwenye maendeleo ya Soka nchini.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic