February 13, 2021


 MABINGWA watetezi Simba, chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes ukuta wake unapa tabu kwa kugaragazwa na ule wa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kwenye kazi kuokota mabao mengi nyavuni ndani ya ligi.

Ikiwa Simba imecheza jumla ya mechi 17 safu yao ya mabeki inayoongozwa na Pascal Wawa imeokota jumla ya mabao 8 nyavuni huku ile ya Yanga inayoongozwa na Lamine Moro ikiwa imeokota jumla ya mabao 7.


Kwenye mechi 17 ambazo Simba imecheza ndani ya uwanja ambazo ni dakika 1,530 umekuwa na wastani wa kuokota nyavuni bao kila baada ya dakika 191. Ule wa Yanga ndani ya dakika 1,620 una wastani wa kuokota bao moja kila baada ya dakika 231.


Mbali na ukuta wa Yanga unaoongozwa na Lamine Moro kuwa imara pia ndani ya dakika 90 haujaruhusu kufungwa mabao zaidi ya mawili tofauti na ule wa Simba ambao uliokota nyavuni mabao mawili kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC kwenye sare ya kufungana mabao 2-2.


Leo Yanga ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Mbeya City ambayo imepania kulipa kisasi Uwanja wa Sokoine kwa kufungwa kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza.


Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Mbeya City ilifungwa bao 1-0 ambapo mtupiaji alikuwa ni Lamine Moro.

7 COMMENTS:

  1. Wewe mwandishi uchwara toa taka taka zako hapa. Watu wanazungumzia mechi za kimataifa wewe unatuletea data za uchochoroni ambazo hazina la maana? Najua umeumia na yaliyotokra congo hivyo unataka kujipoza. Vumilia tuu. Pole sana.

    ReplyDelete
  2. ndugu mwandi ulitamani sana saa hii ungekuwa unaandika habari za matano na kurudia nado...roho inakuuuma...utaishia andika kuhusu rekodi zako za akili ya kitoto...na mwisho wa siku watakao ambao kuanzia jana wameanza weka rekodi wanajulikana..

    JE ILE JANA jijini Kinshasa sio rekodi? jiongeze..Andika hiyo sasa

    ReplyDelete
  3. Yako wapi matamanio ya gongowazi AKA utopolo..Ndiyo tena tusikie kelele za wale Eyimael aliita mbumbumbu kazi kupiga kelele utadhani mbwa na nyani ...baaa baaaa baaa
    matano matano nadoo ndiyo ulikuwa wimbo. tafuteni mwingine..mtakereka sana

    ReplyDelete
  4. Huyu mwandishi boya hajielewi. Tofauti ya magoli aliyookota wawa na yale aliyookota lamine ni goli moja tuu. Sasa hapo ndio kupotezwa mazima? Vipi magoli waliyofunga hizo team difference ni kiasi gani? Kama hakuna cha kuandika si unatulia tuu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hapa anazungumzia mchezaji mmoja mmoja... na mbaya na habari za ndani zisiandikwe..ukilaza gani huo?

      Delete
    2. mnataka* habari..

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic