February 7, 2021

 


OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United ameweka wazi kuwa hawana mpango wa kutwaa taji la Ligi Kuu England ambalo lipo mikononi mwa Liverpool inayonolewa na Jurgen Klopp kwa msimu huu.

Kikosi cha United kimeonyesha kuimarika msimu huu ndani ya uwanja ambapo kimekuwa kikipata matokeo chanya ndani ya dakika 90.

Kauli ya Solskjaer imekuja baada ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 dhidi ya Everton ikiwa ndani ya Old Trafford ambapo United ilianza kufunga kupitia kwa Edinson Cavan dakika ya 24,Bruno Fernandes dakika ya 45 na lile la tatu ni mali ya Scott Mc Tominay.

Everton walipindua meza kibabe kupitia kwa Abdoulaye Doucoure dakika ya 49,James Rodriguez dakika ya 52 na msumari wa kuweka mzani sawa ulipachikwa dakika ya 90+5 na Dominic Calvert-Lewin.

Matokeo hayo yanaifanya United ifikishe pointi 45 ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 23 huku Everton ikiwa nafasi ya 6 na pointi 37 baada ya kucheza mechi 21.

Ole amesema:"Tumecheza vizuri na viwango kwa wachezaji vizidi kuimarika ila ninadhani kwamba kwa wakati huu hatuna hesabu kubwa za kutwaa ubingwa tunaweka nguvu kubwa kujiimarisha zaidi,".

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic