WACHEZAJI wa Yanga wameapa kuibuka na ushindi katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mbeya City utakaofanyika kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Mchezo huo utakuwa wa kwanza kwa Yanga katika mzunguko wa pili wa ligi hiyo ambapo mchezo wa mzunguko wa kwanza baina ya timu hizo, Yanga ilishinda bao 1-0 mfungaji akiwa ni beki Lamine Moro.
Kiungo wa kati wa Yanga, Feisal Salum amesema malengo yao makubwa kuelekea mchezo huo ni kupata matokeo mazuri ambayo ni ushindi jambo ambalo wanaomba liweze kufanikiwa ili kupata ushindi.
“Kikubwa kuelekea mchezo huu ni kupata matokeo mazuri kwa timu ambayo ni ushindi, malengo yetu ni hayo sisi kama wachezaji tutapambania hilo ili liweze kufanikiwa, bila kusahau maombi ya mashabiki wetu ambayo ni muhimu kwetu,” alisema.
Naye beki wa kulia wa Yanga, Kibwana Shomari, alisema: “Msimu huu malengo yetu ni ubingwa, hivyo ni lazima tuweze kukusanya pointi nyingi ikiwemo katika mchezo wetu unaofuata wa ligi dhidi ya Mbeya City, tutapambana kufanikisha hilo.”
Manyani fc mnapigwa
ReplyDeleteMapaka fc Congo tanozina wahusu
ReplyDeleteNguruwe fc mmeenda CONGO kupigwa KHAMSA mapaka fc nyie
ReplyDeleteLeo mapaka fc 0:5 AS VITA
ReplyDeleteWanaitwa "VIMBURU"
ReplyDeleteA.K.A UTOPOLO FC
ReplyDeleteMkumbusheni aliyebeba nyau wenu asimsahau kwa mama ntilie......
ReplyDeleteKwa wema upi unaotutakia kama co kuwanga mchana kweupe
DeleteHapana haja ya kuapa kiapo cha ushindi wakati mnakwenda kucheza na timu ambayo ni ya mwisho imekamata mkia kabisa. Ni sawa kuapa na kujigamba kuwa utamuuwa maiti. Timu hiyo ya Mbeya City inaelekea kuteremka daraja, labda ipite miujiza itayowavuwa
ReplyDelete