February 10, 2021


MTUPIAJI namba moja ardhi ya Bongo anayekipiga ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa ushindani umekuwa mkubwa kwa upande wa Ligi Kuu Bara kiujumla pamoja na utupiaji.


Kagere ni kinara wa mabao akiwa nayo kibindoni 9 na anafuatiwa na mshikaji wake John Bocco mwenye mabao saba huku Adam Adam yupo zake JKT Tanzania akiwafuatia yeye anayo 7.


Bao lake la 9 aliwatungua Azam FC,  Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa kiume uliochezwa Februari 7 wakati timu zote zikigawana pointi mojamoja kutokana na sare ya kufungana mabao 2-2.


Kagere amesema:"Ushindani ni mkubwa na kila mmoja anapenda kufanya vizuri hivyo bado nami nitarudi kupambana,".


Anakazi ya kutetea kiatu cha ufungaji bora alichosepa nacho msimu wa 2019/20 baada ya kutupia mabao 22.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic