MSHAMBULIAJI wa Yanga, Mghana, Michael Sarpong amefunguka kitendo cha kurudi kwao Ghana wakati wa mapumziko kitamsaidia kubadilisha upepo mbaya wa kushindwa kufunga mabao katika Ligi Kuu Bara tangu ajiunge na timu hiyo.
Sarpong amejiunga na Yanga akitokea Rayon Sport ya Rwanda ambapo alifanikiwa kufunga mabao 41 kwa msimu miwili kabla ya kujiunga na Yanga ambayo amefanikiwa kuifungia mabao manne pekee kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi kuu.
Nyota huyo amesema kuwa, amerejea upya baada ya kutoka kwao katika mapumziko mafupi hivyo anaamini ni wakati wake wa kuweza kufanya vizuri katika mzunguko wa pili wa ligi kuu.
“Nirejea nyumbani kwa sababu sikuweza kupata muda awali wa kuweza kwenda kwa sababu nimekuja hapa kutokea Rwanda na wakati ule hakukuwa na usafiri wa kuweza kunipeleka hivyo muda mrefu nilikuwa mbali na familia yangu.
"Nashukuru Mungu, nimerejea kwetu kuona familia yangu, nimekuwa na furaha kubwa kwa kuwa nilipata nafasi ya kushiriki katika matukio ya kijamii kwa kuweza kuwapa chochote jambo ambalo limenizidishia amani moyoni na nimerudi nikiwa mpya kabisa kwa ajili ya kufunga mabao ili kufuta makosa ya mzunguko wa kwanza,” amesema.
Mchezo wao ujao wa mzunguko wa pili ndani ya ligi ni dhidi ya Mbeya City ambao utachezwa Februari 13, Uwanja wa Sokoine Mbeya.
0 COMMENTS:
Post a Comment