February 26, 2021

 


LICHA ya Mtibwa Sugar kuanza kufunga bao la kuongoza mbele ya JKT Tanzania kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora dakika ya 5 kupitia kwa Abal Kassim walikwama kulinda ushindi huo.


Ikiwa Uwanja wa Jamhuri, Morogoro  chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery imekubali kutolewa kwa mikwaju 4-5 ya JKT Tanzania baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.


Bao la kuweka usawa kwa JKT Tanzania lilipachikwa na Daniel Lyanga dakika ya 17 na lile ma pili lilifungwa na Lyanga tena kwa mkwaju wa penalti dakika ya 27.


Mpaka muda wa mapumziko,  Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ulikuwa unasoma Mtibwa Sugar 1-2 JKT Tanzania. 


Bao la usawa kwa Mtibwa Sugar lilipachikwa dakika ya 90 kupitia kwa Issa Rashid, 'Baba Ubaya'dakika ya 90+2 kwa mkwaju wa penalti. 


Mtibwa imefungashiwa virago kwa kufungwa penalti hizo 4-5 ambazo wameshinda wageni JKT Tanzania na kujipatia tiketi ya kutinga hatua ya 16 bora .

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic