February 6, 2021

 


BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji ndani ya Klabu ya Simba amesema kuwa furaha yake ni kuona malengo ya timu hiyo yanatimia hivyo ataendelea kupambana.


Hivi karibuni ilielezwa kuwa nyota huyo raia wa Ghana hawezi kucheza mechi za ushindani atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi sita kwa kuwa anasumbuliwa na Hernia pamoja na majeraha ya muda mrefu.


Taarifa hiyo ilipingwa na Uongozi wa Simba ukiongozwa na Mtendaji Mkuu, Barbara Gonzalez pamoja na Ofisa Habari, Haji Manara. 


Barbara aliweka wazi kuwa Morrison ni mzima na ni mali ya Simba huku Manara akisisitiza kwamba Morrison atacheza Simba Super Cup pamoja na mashindano mengine bila mashaka.


Kwenye Simba Super Cup,  alicheza mechi zote mbili mbele ya Al Hilal alifunga mabao mawili yaliyompa tuzo ya mfungaji bora na alicheza pia mbele ya TP Mazembe.  Februari 4 alicheza mbele Dodoma Jiji ikiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara na alifunga bao moja wakati timu hiyo ikishinda mabao 2-1.


Morrison ambaye amebatizwa jina la mzee wa kukera amesema:"Ninafurahi kuwa ndani ya Simba na malengo ni kuona timu inapata matokeo na kufikia malengo hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic