ZAKARIA Thabit, Ofisa Habari wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa maandalizi kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba yapo vizuri na hawana mashaka yoyote.
Azam FC chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina inatarajiwa kumenyana na Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, kesho Februari 7.
Mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kuwa ndani ya tatu bora kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 32 imecheza mechi 17 na Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 38 imecheza mechi 16,zote zinapambania pointi tatu kupunguza pointi za Yanga ambao wapo nafasi ya Kwanza na pointi zao 44.
Thabit amesema:"Tunazihaitaji pointi tatu za Simba kwa kuwa tunahitaji kurudi Kwenye kasi yetu ile ambayo tulianza nayo awali mzunguko wa kwanza na inawezekana kwa kuwa tuna kikosi imara.
"Morali ya wachezaji ni kubwa na kila mchezaji anahitaji kuonyesha uwezo wake ndani ya uwanja pamoja na mbinu ambazo mwalimu anewapa hivyo hatuna mashaka, mashabiki watupe sapoti, ".
Azam FC inadaiwa pointi 12 na vinara huku Simba ikiwa inadaiwa pointi 6 na vinara jambo ambalo litaongeza ushindani ndani ya dakika 90.
0 COMMENTS:
Post a Comment