BAADA ya mapumziko ya muda wa mwezi mzima kwa Ligi Kuu Bara kutokana na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kushiriki mashindano ya Chan sasa mzunguko wa pili unarejea.
Tumeona kwamba wachezaji ambao
walikuwa wanapeperusha bendera ya Tanzania Cameroon wameshinwa kuwatoa
kimasomaso Watanzania kwa kusonga mbele hatua ya robo fainali.
Imani yangu ni kwamba kuna kitu
ambacho wamejifunza na kujua kwamba yale makosa ambayo waliyafanya awali
watakuwa imara wakati ujao. Kwenye mpira hakuna namna ya kubadili matokeo hivyo
lazima tukubali kwa sasa.
Kikubwa ni kukubali kujipanga upya
kwa ajili ya wakati ujao ili timu iweze kupata matokeo mazuri na kuendelea
kupeperusha bendera ya Tanzania.
Licha ya kuondolewa kwenye hatua ya
makundi bado vijana walipambana kusaka ushindi ila bahati haikuwa upande wao.
Watanzania wanastahili pongezi kwa sapoti yao ambayo wamekuwa wakiitoa kwa
Stars.
Pia ni fundisho kwa Stars kujua
kwamba Tanzania inapenda kuona matokeo ila yote yanawezekana hivyo cha muhimu
ni kujipanga na kufanya vizuri wakati ujao.
Mzunguko wa pili una ushindani mkubwa hilo lipo wazi hivyo ni muhimu kwa timu kujipanga kufanya vizuri.
Wakati huu wa mzunguko wa pili ni
muda wa kukamilisha hesabu kwa kila timu ambayo ilishindwa kuchanga karata zake
vyema kutokana na matokeo ambayo iliyapata ndani ya uwanja.
Kuanzia zile ambazo zinapambania
kusepa na taji la Ligi Kuu Bara zile ambazo zinapambania kubaki ndani ya Ligi
Kuu Bara pamoja na zile ambazo zinapambana kupanda Ligi Kuu Bara.
Ipo wazi kwamba mwisho wa ligi kuna
timu ambazo zitashuka daraja ambapo ikiwa zitashindwa kupambana wakati huu njia
yao ipo wazi.
Zile za Ligi Daraja la Kwanza
ambazo zitapata matokeo mazuri ni wakati wao wa kupanda mpaka kwenye ligi kuu
kuendelea kupambana kwa ajili ya maisha mengine ya ushindani.
Ni furaha kubwa kwa timu kupanda
ligi huku huzuni kubwa ikiwa ni kwa zile ambazo zitashuka ligi kutokana na
ushindani ambao huukuta pale wanaposhuka ligi daraja la kwanza.
Jambo la msingi ni kila timu kwa
sasa kujipanga kwenye mechi zilizobaki ili kupata matokeo chanya ambayo
yatawapa pointi tatu zitakazowafanya waweze kubaki ndani ya ligi msimu
ujao.
Kuna dakika 90 ndani ya uwanja kwa
ajili ya kusaka pointi tatu ambazo ni muhimu kwa kila timu iliyojiwekea
malengo makubwa.
Sapoti ambayo timu inapata kutoka
kwa mashabiki ni muhimu kulipwa ndani ya uwanja.Kila timu kwa sasa inahitaji
kumaliza ligi kwa mafanikio hivyo muda wa mwisho kujipanga ni sasa.
Kwa mechi hizi za mwisho pia ni
muhimu kwa waamuzi kuendelea kufanya vizuri zaidi kwa kuzingatia sheria za
mpira ili kuona kwamba kila timu inashinda bila malalamiko.
Wachezaji nao pia ndani ya uwanja
kazi yao ni kupambana kusaka ushindi kwa haki bila kuchoka na kufuata sheria za
mpira.
Ni dakika 90 ambazo zitaamua hatma
ya timu ndani ya uwanja pamoja na nafasi ya timu hiyo kwa kuwa pointi
zinapatikana kwa ushindi pekee.
Juhudi ni muhimu kwa wachezaji na
kuzingatia nidhamu nje na ndani ya uwanja hiyo ni njia sahihi kwa timu kuweza
kupata matokeo mazuri.
Matokeo mazuri ndani ya uwanja pia
yanategemea maandalizi mazuri hivyo muda ambao umebaki kwa sasa kabla ya ligi
kuendelea utumike vizuri kwa ajili ya maandalizi.
Maandalizi mazuri ni silaha ya timu
kupata matokeo mazuri kwenye mechi zote kwani hapo ndipo ambapo mwalimu hupata
kikosi cha kazi pamoja na kujua namna gani awatumie wachezaji wake.
Ligi yetu imezidi kufuatiliwa na
wengi jambo ambalo linaamnisha kwamba hatupo nyuma sana kwenye kukua hivyo ni
kazi kwa wachezaji pia kulitambua hilo.
Ikiwa wataongeza pia juhudi ni
rahisi kwao kuweza kutusua na kupata changamoto mpya nje ya Bongo kwani kwa
sasa soka imekuwa biashara.
Pia mbali na Stars kuna Ligi ya
Wanawake nayo pia imekuwa ikendelea na ushindani huku ni mkubwa kwa kila timu
kuwa na nia ya kufanya vizuri ndani ya uwanja.
Kwa zile ambazo zilikuwa zinakwama
kupata matokeo ndani ya mechi zao ambazo wamecheza ni wakati wao wa kujipanga
upya na kuanza kwa namna nyingine.
Tusisahu pia kuna Ligi ya Wanawake
ambayo inaendelea kushika kasi na kila siku ushindani unazidi kukua kwa kasi
huku pia.
Timu zote nazo zinaingia kwenye
mzunguko wa pili ambao ni muda wa kukamilisha ile ngwe ya kwanza iliyoanza na
hapa ndipo ambapo bingwa atakwenda kupatikana.
Kila la kheri timu zote kwenye
maandalizi ya mzunguko wa pili na imani yangu ni kwamba kila kitu kitakwenda
sawa.
0 COMMENTS:
Post a Comment