February 6, 2021

 


BAADA ya kupoteza mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC, Namungo inawavutia kasi wapinzani wao Ruvu Shooting inayonolewa na Charles Mkwasa kwenye mchezo wao wa ligi utakaochezwa kesho, Februari 7.

Namungo inayonolewa na Hemed Morocco ilifungwa mabao 3-0, Uwanja wa Uhuru na kuyeyusha pointi tatu jumlajumla.

Kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya 15 ikiwa na pointi 15 ikiwa imecheza jumla ya mechi 15 kwa msimu wa 2020/21.

Ina wastani wa kusepa na pointi moja kwenye kila mchezo ambao inaingia ndani ya uwanja msimu huu.

Inakutana na Ruvu Shooting ambayo ipo nafasi ya tano na pointi zake ni 28 baada ya kucheza jumla ya mechi 17.

Haijawa kwenye mwendoo wa kuvutia kwa msimu wa 2020/21 tofauti na msimu wa 2019/20 jambo ambalo linampa wakati mgumu Kocha Mkuu, Hemed Morroco kurejesha makali ya timu hiyo.

Morroco amesema kuwa anaamini watafanya vizuri kwenye mechi zao zilizobaki ili kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.

"Ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo chanya hivyo ni wakati wa kujipanga upya kutumia makosa kupata matokeo chanya,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic