February 5, 2021


MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze, Fiston Abdul Razack amesema kuwa huwa hadumu kwa muda ndani ya timu nyingi kutokana na kupewa ofa kila wakati.

Ingizo hilo jipya kutoka nchini Burundi rekodi zinaonyesha kuwa amekuwa akikaa na timu kwa muda mfupi jambo ambalo linatoa picha kwamba atasepa pia ndani ya Yanga.

Miongoni mwa timu ambazo amcheza mwamba huyo ni pamoja na 1 de Agosto msimu wa 2017. Al Zawraa msimu wa 2018, JS Kabylie msimu wa 2018-19 na ENPPI msimu wa 2019-20.

Amesaini dili la miezi sita lenye kipengele cha kuongeza mkataba ndani ya timu hiyo inayoongoza ligi ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18.

Fiston amesema:"Nimekuwa nikipata ofa nyingi kila nikiwa kwenye timu jambo ambalo linanifanya nisiweze kudumu mahali ambapo huwa ninakuwa.

"Kikubwa ni kuona kwamba timu inapata mafanikio na kila mmoja analijua hilo, nipo sehemu sahihi na kila mchezaji anafurahia uwepo wangu ni imani yangu kwamba tutafikia malengo ambayo tumejiwekea," amesema.

Anaungana na kiungo mshambuliaji Said Ntibanzokiza ambaye ni raia wa Burundi kama yeye.



5 COMMENTS:

  1. Huyo inawezekana katishwa na Amisi Tambwe yaliyomfika yeye na wengi kabla yake ya kutolipwa haki zake hadi kutinga FIFA yameshamshituwa

    ReplyDelete
  2. Mchezaji anayeaminiwa hawezi kupewa mikataba mifupi hivyo Wala hawez kuhamahama kila wakati

    ReplyDelete
  3. ukitazama player profile katik TRANSFER MARKET UTAPA MAJUBU SAHIHI KUWA ANADANGANYA

    ReplyDelete
  4. Hata timu ya taifa hayupo halafu aseme Ana ofa lini na wapi anazingua tuuuu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic