February 5, 2021

 



KIUNGO mshambuliaji wa klabu ya Yanga, Said Ntibazonkiza 'Saido' amefunguka kuwa  mshambuliaji mpya wa klabu huyo Fiston Abdoul Razak atafanya mambo makubwa ndani ya kikosi cha klabu hiyo kutokana na uwezo mkubwa alionao.

Fiston alikamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Yanga katika dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15, mwaka huu na tayari amekabidhiwa jezi namba saba kwa ajili ya kukiwasha ndani ya timu hiyo.

Saido na Fiston wamekuwa wakicheza pamoja mara kwa mara katika kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi, ambapo kutokana na uwezo mkubwa wanaouonyesha wamekuwa wakitajwa kama wachezaji mapacha.

Akizungumzia uwezo wa Fiston, Saido amesema: "Ni muda mrefu sasa nimefanikiwa kuwa karibu na Fiston na tumekuwa tukicheza pamoja kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi, hivyo najua yeye ni mchezaji wa kiwango cha juu na najisikia furaha kupata nafasi ya kucheza naye kwenye kikosi cha klabu ya Yanga.

"Naamini tutaonyesha uwezo mzuri pamoja kwa ajili ya kuisaidia Yanga iweze kufikia malengo yake ya kutwaa ubingwa msimu huu,"

 


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic