February 4, 2021


DIDIER Gomes,  Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wamepambana kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Dodoma Jiji, jambo ambalo wanahitaji pongezi. 


Ikiwa Uwanja wa Jamhuri Simba imeshinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji kwenye mchezo wa Kiporo na kusepa na pointi tatu.

Bao la kwanza kwa Simba lilipachikwa na Meddie Kagere dakika ya 30 likawekwa usawa na Cleophance Mkandala dakika ya 36 ambaye alionyeshwa kadi ya njano kwa kushangilia akiwa ametoa jezi.


Bernard Morrison ambaye aliweza kuanza kwenye mchezo wa kwanza wa Gomes ndani ya Simba katika Ligi Kuu Bara alipachika bao ushindi dakika ya 66 kwa pasi ya Perfect Chikwende. 


Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 38 ikiwa imeachwa kwa pointi 6 na watani zao wa jadi Yanga wenye pointi 44 wakiwa nafasi ya kwanza.

Gomes amesema:"Wachezaji wamepambana kutafuta pointi tatu wanahitaji pongezi hesabu zetu ni mchezo wetu ujao wa Ligi Kuu Bara, ".


Februari 7 Simba itashuka Uwanja wa Mkapa kusaka pointi tatu mbele ya Azam FC inayonolewa na George Lwandamina. 


Mbwana Makata, Kocha Mkuu wa Dodoma Jiji amesema kuwa wachezaji wake wamecheza kwa nidhamu licha ya kupoteza mchezo wa leo.


7 COMMENTS:

  1. Mimi Nina Swali kwanza hongera Simba kwa ushindi,Sasa Swali ni nimekuwa/na tumekuwa tukiangalia Soccer /Football achilia mbali Kutangaza mchezo Kama mchezo kwanini ma pundits/game analyzers kwetu hapa TFf not Tanzania ni watu tofauti na Uchezaji wa mpira kwa maana ya kuujua na kuushiriki kimwili na kiakili kama siyo kiroho ama ukilinganisha na Dunia ya Soka, je Tanzania inawezekana tunajua njia za michezo kuliko Dunia Ile yote

    ReplyDelete
  2. Nawapongeza simba kwa ushindi. Muhimu waongeze kasi na pasi za kwenda mbele. Viporo viliwe vyote tuanze upya

    ReplyDelete
  3. Hongereni sana Simba.
    Naombeni ufafanuzi wa kanuni za ligi kuu Bara kwa wachezaji wa kigeni ni wachezaji wangapi wa kigeni wanatakiwa kucheza kwenye mchezo mmoja. Mana kanuni za ligi kuu sura 52 inasema wachezaji wa kigeni wasizidi sita kwa mchezo mmoja lakini kwa Mchezo wa Dodoma Fc na Simba nimeona wachezaji wa kigeni kwa simba walizidi.
    Naombeni tafsiri sahihi ya hiyo kanuni yawezekana sijaielewa vizuri.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Subiri watakuja ila kwa sasa tujipongeze kaa ushindi

      Delete
    2. Kanuni zinabadilika kila msimu kwahyo kwasasa hata ukianzisha wote wa kigeni hakuna shida

      Delete
    3. Acheni vijisababu mwenyenafasi anakuja kaa chonjo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic