BAADA ya kufanikiwa
kutupia kambani mabao manne katika michezo mitatu iliyopita, Straika wa Dodoma
jiji Anuary Jabir ametamba kuwa mabao hayo yamezidi kumpa morali ya kufanya
vizuri, ili kutimiza malengo yake ya kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara.
Jabir aliifungia Dodoma Jiji mabao mawili katika mchezo uliopita dhidi ya Polisi Tanzania ulioisha kwa sare ya mabao 2-2.
Msimu uliopita akiwa na
kikosi cha Dodoma Jiji kwenye Ligi Daraja la Kwanza (FDL), straika huyo
aliibuka mfungaji bora wa michuano, hii ni baada ya kuweka kambani mabao 11.
Akizungumzia malengo yake Jabir amesema: “Mchezo uliopita dhidi ya Polisi Tanzania ulikuwa
na ushindani mkubwa, nashukuru kwa kuweza kufunga mabao mawili yaliyoipa timu
yangu matokeo ya sare.
“Nimefunga mabao manne
katika michezo mitatu iliyopita, kama mshambuliaji ninayechipukia hili linazidi
kunipa moyo katika ndoto zangu za kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu,”
Sare hiyo imewafanya
Dodoma jiji kufikisha pointi 29 katika michezo 21 waliyocheza mpaka sasa wakiwa
katika nafasi ya saba ya msimamo wa ligi







Kanjanja fanya editing Anwar anachezea JKT au Dodoma Jiji?
ReplyDelete