February 25, 2021

 



BAADA ya kufanikiwa kutupia kambani mabao manne katika michezo mitatu iliyopita, Straika wa Dodoma jiji Anuary Jabir ametamba kuwa mabao hayo yamezidi kumpa morali ya kufanya vizuri, ili kutimiza malengo yake ya kuibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara.

Jabir aliifungia Dodoma Jiji mabao mawili katika mchezo uliopita dhidi ya Polisi Tanzania ulioisha kwa sare ya mabao 2-2.

Msimu uliopita akiwa na kikosi cha Dodoma Jiji kwenye Ligi Daraja la Kwanza (FDL), straika huyo aliibuka mfungaji bora wa michuano, hii ni baada ya kuweka kambani mabao 11.

Akizungumzia malengo yake Jabir amesema: “Mchezo uliopita dhidi ya Polisi Tanzania ulikuwa na ushindani mkubwa, nashukuru kwa kuweza kufunga mabao mawili yaliyoipa timu yangu matokeo ya sare.

“Nimefunga mabao manne katika michezo mitatu iliyopita, kama mshambuliaji ninayechipukia hili linazidi kunipa moyo katika ndoto zangu za kuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu,”

Sare hiyo imewafanya Dodoma jiji kufikisha pointi 29 katika michezo 21 waliyocheza mpaka sasa wakiwa katika nafasi ya saba ya msimamo wa ligi

 

1 COMMENTS:

  1. Kanjanja fanya editing Anwar anachezea JKT au Dodoma Jiji?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic