February 2, 2021

 


 

KIWANGO bora kilichoonyesha na Simba kwenye michuano ya Simba Super Cup kimezifanya klabu shiriki za michuano hiyo, TP Mazembe na Al Hilal kuivulia kofia Simba na kukiri kweli kikosi hiko kiko cha mabingwa wa Ligi Kuu Bara kiko vizuri.

Katika michuano hiyo iliyoanza kutimua vumbi Januari 27, na kufikia tamati Januari 31 Simba iliibuka bingwa baada ya kujikusanyia pointi nne katika michezo miwili waliyocheza.

Michuano hiyo, ilifanyika kwa lengo la kuziandaa timu shiriki na michezo ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Akizungumzia kiwango cha Simba, Kocha mkuu wa Al Hilal Zoran Mamic amesema: “Tulipoteza mchezo wetu wa kwanza dhidi ya Simba kwa mabao 4-1, licha ya kwamba kikosi chetu kiliwakosa nyota kumi wa kikosi cha kwanza na pia tulichelewa kufika Tanzania lakini ni wazi tunapaswa kukiri kuwa Simba walikuwa bora dhidi yetu.

“Wana kikosi kizuri, na faida ya kucheza nyumbani iliwabeba zaidi, namini watafanya vizuri kwenye michezo yao ya Ligi ya mabingwa Afrika.

Naye mwakilishi wa benchi la ufundi la TP Mazembe Kabongo Ngadu alisema: “Tulipata nafasi ya kuutazama mchezo kati ya Simba na Al Hilal na pia kucheza dhidi yao, nikiri kuwa wana kikosi kizuri,"

1 COMMENTS:

  1. Hapa mashabiki wa simba umwatuliza, hivi ndivyo wanavyotaka, gubu kwishiney

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic