February 2, 2021


 MSHAURI ndani ya Klabu ya Yanga kuelekea kwenye mfumo wa mabadiliko, Senzo Mazingisa leo Feburuari 2, 2021 ametaja sababu tatu za klabu yao kuandaa siku maalum ya vyombo vya habari katika kambi yao ya AVIC Town iliyopo Kigamboni jijini Dar es Salaam.

 

Senzo amesema sababu ya kwanza ni kutoa fursa kwa wanahabari kujua na kuzungumza mambo ya mahusiano kati ya klabu yao na wadhamini wao.

 

“Siku zote Yanga ikicheza nafasi ya kuzungumza huwa kwa makocha, wachezaji wanafanya vizuri na kama ukiwa na bahati utaongea na nahodha.


“Leo ni tofauti nawaona wawakilishi wa wadhamini wetu SportPesa, GSM, Afya, Taifa Gas muwaulize leo kwanini wanaidhamini Yanga na kuendelea kuwapa pesa.

 

"Senzo amesema sababu ya pili ni kutoa nafasi kwa waandishi kujua mazingira ya kambi yao iliyopo Kigamboni na kujua mazingira yake na tatu ni kuzidisha umoja kati ya Yanga na Waandishi wa Habari na kuwa karibu na mashabiki," .


7 COMMENTS:

  1. Hivi hii kitu manufaa yake ni yapi hasa kwa club? Kwa anaefahamu vizuri

    ReplyDelete
  2. Yaani kuna vitu vingine unavifanya vinazidi kuluonyesha jinsi ulivyokosa ubunifu. Sioni mantiki

    ReplyDelete
  3. Kupata habari za uhakika za team husika kupitia chanzo husika kama Management na wadhamini, ndio manufaa yake, wamefanya vzr ndio mwanzo au mnataka habari za kuungaunga?

    ReplyDelete
  4. Hii si Yanga tu ndio wameanza kufanya hata vilabu vya Ulaya wanafanya, mfano Chelsea Fc au Arsenal n.k: https://www.arsenal.com/news/behind-scenes-premier-league-media-day

    ReplyDelete
  5. Hivi mikia muko kama msemaji wenu mengine sio lazima mubeze kaeni kimya ila kila jambo akili fanya yanga mbona nyie mumefanya ya kwenu acheni ushamba manufaa ayajuwa yanga sio nyie utelembwe

    ReplyDelete
  6. Vilabu vya ulaya vinafanya sababu mastaa wao ni ngumu Sana kuonana nao hufanya hivyo ili kutoa fursa ya kuonana nao... Je kwa hapa kwetu pia iko hivyo au tunaiga tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic