February 5, 2021


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kuna umuhimu wa wapinzani wao Simba kujipanga wakati mwingine ikiwa wataandaa mashindano kama ya Simba Super Cup.

Januari 27 Simba Cup ilianza na ilishirikisha timu tatu ambazo ni Simba wenyewe wenyeji, Al Hilal na TP Mazembe na bingwa wa mashindano hayo alikuwa ni Simba.

Mechi zote tatu zilichezwa Uwanja wa Mkapa ambapo mchezo wa kwanza Simba ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal na mechi ya pili iliazimisha sare ya bila kufungana na TP Mazembe.

Fredrick Mwakalebela, Makamu Mwenyekiti wa Yanga amesema kuwa ni muhimu kwa mabingwa hao wa Simba Super Cup kujipanga wakati mwingine ili kufanya vizuri.

"Ninakubali kwamba wameandaa Simba Super Cup ila ilibidi wajipange na kufanya tathimini wakati mwingine, yaani umechukua kombe mwenyewe, kombe umeliaandaa mwenyewe.

"Upande wa tuzo binafsi nazo pia unajipa mwenyewe kuanzia mchezaji bora wako, mfungaji bora tena mabao yenyewe mawili, haikuwa inahitajika
hiyo iwepo.

"Wajifunze baadaye kwamba sio lazima kuipa timu yako kipaumbele katika mambo ambayo umeyaandaa kisa wewe ni muadaaji," .

TP Mazembe ni mshindi wa tatu na Al Hilal ni mshindi wa pili kwenye mashindano hayo ambayo yalikuwa ni ya kwanza kwa mrithi wa mikoba ya Sven Vandenbroeck, Didier Gomes.

14 COMMENTS:

  1. Kwa hiyo Simba ilitakiwa ihakikishe haichukui kombe, sio? Morrison alitakiwa asifunge magoli mengi ili asiwe mfungaji boa, sio? Kakolanya alitakiwa asizuie michomo mingi na arhusu mabao mengi ili asiwe golikipa bora, sio? Bwalya alitakiwa asicheze kwa kiwango kikubwa ili asiwe mchezaji bora wa mashindano, sio? Miquisonne alitakiwa asicheze kwa kiwango kikubwa katika mechi ya Mazembe ili asiwe man of the match, sio?

    ReplyDelete
  2. Uongozi uliupataje wewe Utopolo mpaka akili utopolo nini kinachokuuma kwahiyo ungepewa wewe ambaye hukushiriki

    ReplyDelete
  3. ww mwakalebela ulitaka aliyefunga goli moja ndo awe mfungaji bora? na nikukumbushe tu timu iliyofanya vizur ndo mara nying hutoa wachezaji walofanya vzur kuliko woteeeeee

    ReplyDelete
  4. ww mwakalebela ulitaka aliyefunga goli moja ndo awe mfungaji bora? na nikukumbushe tu timu iliyofanya vizur ndo mara nying hutoa wachezaji walofanya vzur kuliko woteeeeee

    ReplyDelete
  5. Sasa wanapotoka tena sana kwasababu lugha yao sasa haina miguu wala vichwa kikubwa nanyi kwanini hamkuomba mechi ya kujipima kama vile Azam eti kila kitu mmejipa wenyewe. Pili pili msiozila zinakuwashieni nini. Kuna mmoja humuhumu alitabiri kuwa matopolo kama kawaida nao wataigia na ni kweli siku yapili wakataja na wao Wananchi Day lakini hawajasema lini bila ya shaka Mkwanja kuliko ule alioutaka Bwalya na huku wakimraja Konde Boy na Tambwe kuwakalia rohoni. Tutashuhudia mengi

    ReplyDelete
  6. Kama kulikuwa na vigezo viliwekwa na hao walipewa nduo walistahili sioni tatizo hapo. Labda tuombe next time wakiandaa waialike na yanga au wamwalike mwakalebela awe msimamizi wa hayo mashindano ili atende haki zaidi

    ReplyDelete
  7. Nimeamini Yanga pale juu kuna viongozi wanatuhujumu

    ReplyDelete
  8. Wanakujumu wewe unanini unajifanya kinyonga wakati wewe ni mjusi nani hakujui kuwa wewe ni mkia mambo ya wanainchi wachie wanainchi utazalishwa mapema wewe mtoto wa kiume

    ReplyDelete
  9. Replies
    1. Matahira fc kuanzia viongozi Hadi washabiki wote ni matahira

      Delete
  10. Ukweli utabaki kuwa ukweli tu Simba wamejitekenya wenyewe na wanackeka wenyewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Chomoa ukimbie Kama inauma,This is Simba mtanuna sana na bado Kama miaka 5 tutakuwa tunawaachia kombe la mapinduzi tu mhangaike nalo teh teh teh

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic