February 5, 2021


AZAM FC, inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina imeendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mechi zake za Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na mchezo wao ujao dhidi ya Simba.

Kuelekea kwenye mchezo huo ambao umeteka hisia za mashabiki wengi tayari mitambo ya mabao ya Azam FC tayari imeanza kazi kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ayoub Lyanga mwenye mabao manne ambaye alikuwa na timu ya Taifa ya Tanzania iliyokuwa Cameroon ikishiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa ndani,(Chan) amerejea mazoezini.

Pia Prince Dube ambaye alikuwa nje ya uwanja kutokana na majeraha ya mkono akiwa na mabao sita na pasi nne za mabao tayari amesharejea na kuanza mazoezi pamoja na kucheza mechi za kirafiki.

Jumla nyota hawa wawili wamehusika kwenye mabao 14 kati ya 24 yaliyofungwa na timu hiyo.

Tayari kikosi kinaendelea na mazoezi Uwanja wa Azam Complex kipo nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zake kibindoni ni 32 baada ya kucheza jumla ya mechi 17.

Kinakutana na Simba ambao wapo nafasi ya pili na pointi zao ni 38 baada ya kucheza jumla ya mechi 16.

Lwandamina amesema kuwa wanaamini utakuwa mchezo mgumu ila watapambana kupata matokeo ndani ya uwanja.

Didier Gomes Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ili kuweza kupata matokeo chanya.

Ushindi wa Azam FC utawaongezea nguvu kuendelea kufukuza malengo ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara sawa na Simba ambao ni mabingwa watetezi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic