February 6, 2021

 


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi leo, Februari 6 Uwanja wa Azam Complex kushuhudia mchezo wa kirafiki kati yao dhidi ya African Sports ya Tanga.


Ikiwa ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo na pointi zake 44 ndani ya Ligi Kuu Bara, leo itacheza mchezo wa kirafiki kujiweka fiti tayari kwa ajili ya mwendelezo wa mechi za ligi.


African Sports inashiriki Ligi Daraja la Kwanza nayo pia itakuwa inajiweka sawa kwa ajili ya mwendelezo wa ligi pamoja na mashindano mengine. 


Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa ni muda wa mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia burudani kutoka kwa vinara wa ligi.


"Tutatoa burudani na kile ambacho kimekosekana kwa muda ndani ya uwanja hasa baada ya kukaa muda mrefu bila kucheza.


"Maandalizi yako vizuri na imani yetu ni kutoa burudani safi pamoja na matokeo chanya kwa mashabiki wetu kuanzia saa 1:00 usiku, usikubali kukosa,".


Yanga ilianza mazoezi rasmi Januari 25 chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye ndani ya ligi  ana tuzo mbili za kuwa kocha bora zinazotolewa na Kamati ya Tuzo iliyo chini ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

4 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic