MSHAMBULIAJI wa AS Vita, Ducapel Moloko, amewapiga mkwara mzito Simba kwa kusema kuwa watachukua alama tatu watakapokutana uwanjani Jumamosi hii.
Kauli hiyo ameitoa zikiwa zimebaki siku chache kabla timu hizo hazijavaana kwenye mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.
Moloko amesema kuwa, wamejipanga kuchukua ushindi kwa Simba ili kutengeneza nafasi ya kufuzu hatua ya makundi.
“Sisi tumejiandaa na tutaifunga Simba ikiwa nyumbani kwao na alama zote tutazichukua, subiri tuje mtauona moto wetu,” alisema mshambuliaji huyo.
Katika michuano hiyo, Simba ndiyo vinara wa Kundi A wakiwa na pointi 10, wakifuatiwa na Al Ahly yenye saba, huku AS Vita ikijikusanyia pointi nne na Al Merrikh moja.
Timu zote zimecheza mechi nne zikibakiwa na mbili kukamilisha hatua hiyo kabla ya kwenda robo fainali ambapo Simba inahitaji pointi moja ili kuweza kutinga hatua hiyo.
Mwambie ajiandae kutoa machozi kwa mkapa hatoki mtu🤣🤣🤣🤣🤣
ReplyDeleteAtafungwa nyingi hajawahi fungwa ����������������
ReplyDeleteAtulie huko watu tuko bize kujiandaa na hilo game
ReplyDeleteMkawapokee. Naona unawependa Sana.
ReplyDeleteNa hivi tunamachunga aje polepole ataumia nyingi
ReplyDeleteMtaambiwa wachezaji 8 wana CORONA mtashindaje?
ReplyDeleteNjoo tukupe corona ukakae quarantine
ReplyDelete🤣🤣🤣🤣
ReplyDeleteMwisho wa mchezo anapo hojiwa asijesema mpira unamatokeo matatu maana hicho kisingizio tumekizoea na kinajulikana.
Siku hizi mpira siyo maneno .mpira ni mapambano ya dakika 90. Wajipange kwani kesho ni Siku mbaya sana Kwa as vita. Maana wana mgandamizo wa kupata matokei.
ReplyDelete