THABIT Zakaria, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa muda wa mapumziko kwa wachezaji wa timu hiyo umekwisha hivyo wanarejea mazoezi kuanza kazi ya kulikimbizia jambo lao waliloanza nalo mwanzoni mwa msimu wa 2020/21.
Wachezaji wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina walipewa mapumziko kutokana na maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 17.
Akizungumza na Saleh Jembe, Zakaria amesema kuwa tayari muda ambao waliwapa wachezaji kwa ajili ya mapumziko umekwisha hivyo wamerejea kuanza kufanya mazoezi.
“Tupo salama na tunahitaji kutimiza jambo letu. Kwa sasa tumeanza mazoezi kwa kuwa muda ambao tulitoa kwa ajili ya mapumziko kwa wachezaji umekwisha,” amesema.
Kwenye msimamo wa ligi, Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa imecheza jumla ya mechi 24 ina pointi 44 kibindoni kinara ni Yanga mwenye pointi 50 baada ya kucheza mechi 23.
Kweli ndoto hizi ni noma
ReplyDelete