March 30, 2021

 


FLORENT Ibenge, Kocha Mkuu wa AS Vita amesema kuwa watapambana kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao dhidi ya Simba ili waweze kutimiza malengo ya kutinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

AS Vita inakumbuka kwamba ilipokutana na Simba mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika ubao ulisoma AS Vita 0-1 Simba.

Bao lililowapa Simba pointi tatu lilifungwa na Chris Mugalu kwa mkwaju wa penalti na kuwafanya wasepe ugenini wakiwa kifua mbele.

Kwenye msimamo wa kundi A, AS Vita ina pointi nne huku Simba ikiwa na pointi 10 inaongoza kundi inafuatiwa na Al Ahly nafasi ya pili yenye pointi 7.

Imekuwa ikipata matokeo ugenini AS Vita kwa kuwa pointi zote nne ilikusanya ugenini ilishinda mbele ya Al Merrikh inayoshika nafasi ya nne na pointi moja na ililazimisha sare mbele ya Al Ahly.


Ibenge amesema:"Tunahitaji kushinda mchezo wetu ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu uhitaji wetu ni kuona kwamba tunaweza kutinga hatua ya robo fainali.

"Wapinzani wetu Simba wakiwa nyumbani wapo vizuri ila nasi pia tutajipanga kupata matokeo mazuri ili tufikie malengo yetu,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic