March 30, 2021

 


KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa maendeleo ya nyota wake ambao walikuwa wakisumbuliwa na majeraha ikiwa ni pamoja na Mapinduzi Balama, Dickson Job yamezidi kuimarika.

Job alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja ambayo aliyapata kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ila kwa sasa amerejea kwenye ubora wake na kuanza mazoezi.

Balama alikuwa nje kwa muda mrefu akitibu majeraha ya kisigino aliyoyapata msimu wa 2019/20 aliyoyapata kwenye mazoezi ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara ilikuwa dhidi ya Ndanda FC.

Tayari naye ameanza kupewa program maalumu ambayo itaweza kumrejesha uwanjani kuendelea na majukumu yake.

Mwambusi amesema:"Kila mchezaji anaonekana kuwa na furaha na taratibu wale ambao hawakuwa fiti wanarudi, Mapinduzi Balama amepewa program maalum huku wachezaji wengine wakiwa wameanza mazoezi.

"Fiston naye kwa sasa anaendelea vizuri ni jambo jema kwetu na tunaamini wale wengine ambao hawajawa kwenye ubora wataimarika," .

Yanga inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza mechi 23 inafuatiwa na Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes ipo nafasi ya pili na pointi 46 baada ya kucheza mechi 20.

Imeanza mazoezi ikiwa na nyota wake ambao ni pamoja na Paul Godfrey, Yacouba Songne, Ramadhan Kabwili, Kibwana Shomari.

 

5 COMMENTS:

  1. Ubingwa wa ligi kuu bara msimu huu hautabiriki,labda yanga akate tamaa mapema

    ReplyDelete
    Replies
    1. ENDELEA KUJIFARIJI ILA KIMBUNGA KINAKUJA,WAKIRUDI UWANJANI WATUMENI WAJE KUKAMIA MECHI TENA UONE KITAKACHOWAPATA,UNAFIKIRI KWANIN WACHEZAJI WA NDANI NDIO WANAOONGOZA KWAKUPATA MAJERAHA? KWASABABU WANAKAMIANA MECHI HAWACHEZI MPIRA WA KIWANGO WALICHONACHO WANALAZIMISHA ILI WAONEKANE HATIMAE NDIO HAYO YAKUPATA MAJERAHA YANAYOWAWEKA NJE YA UWANJA MUDA MREFU NA KADI ZISIZO NA TIJA, YANGA KUA BINGWA TAYARI MBONA ISIPOKUA SIO KWA MSIMU HUU, KWANZA ATAKUFA MBELE YA PRISON AKIJA LIGI KUU ATASULUHU SANA NA ATAPOTEZA VILEVILE, KWENYE ALAMA 30 ALIZOBAKISHA ATAVUNA HAPO ALAMA 20-25 TU JUMLA ATAKUWA NA ALAMA 70-75 MPAKA LIGI YAISHA HUO NDIO UTAKUA MSIMAMO WA YANGA MSIMU HUU.SIMBA AMEBAKISHA 39 HAPO ATACHUKUA ALAMA 30-32 JUMLA ATAKUA NA ALAMA 76-78 MPAKA LIGI ITAKAPOISHA SASA KAMA UMEKAA NA WENZAKO MKAJIDANGANYA SUBIRI UONE KITAKACHOTOKEA.

      Delete
    2. Wachezaji wengi wanaoumia ndio wanaokamiwa kwa ajili ya ubora wao na sio wakamiaji...Mr. kilaza.

      Delete
  2. Huyu dogo mapinduzi ndio atapindua meza Mwenyewezi Mungu amuwezeshe kuafiti, ni mchezaji mzuri kuliko hata baadhi ya Wachezaji wa nje.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakubaliana nawe ndugu. Anachezesha timu fresh na anafunga pia. Nilimmiss sana uwanjani.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic