March 22, 2021


 KOCHA Mkuu wa AS Vita, Florent Ibenge amesema kuwa ili waweze kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika wanatakiwa kuibuka na ushindi katika michezo yao miwili iliyosalia ya ligi hiyo, dhidi Simba na Al Merrikh.

 

AS Vita kwa sasa inashika nafasi ya tatu katika kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika mara baada ya kujikusanyia pointi 4 nyuma ya Simba wenye 10 na Al Ahly wana saba.


 Kocha Ibenge amesema kuwa kulingana na matokeo na pointi ambazo wamezipata wanatakiwa kushinda michezo yao miwili ijayo bila kujali wanakutana na timu ipi kwani wasipofanya hivyo hawatakuwa na uwezo wa kusonga mbele kuelekea katika hatua ya robo fainali.

 

“Tunatakiwa kushinda michezo yetu yote miwili iliyosalia dhidi ya Simba na Al Merrikh ili tuweze kusonga mbele katika hatua ya robo fainali, matokeo tuliyopata hayakuwa mazuri sana kwetu lakini huu si muda wa kulaumiana tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha tunasonga mbele.

 

“Tunatakiwa kutojali tunacheza na mpinzani wa aina gani, michezo yote iliyosalia ni migumu kwetu tunacheza na Simba tukiwa ugenini mara ya mwisho tulipoteza mchezo pale hivyo hatutakiwa kurudia makosa, mchezo wa mwisho tutakuwa nyumbani kila mtu anafahamu hatujashinda hata mchezo mmoja kwetu pia tunatakiwa kurekebisha hili,” amesema kocha Ibenge.

 

AS Vita wanatarajia kucheza na Simba ugenini Aprili 3, katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar huku mchezo wa mwisho ukitarajiwa kufanyika DR Congo Aprili 9 dhidi ya Al Merrikh.

6 COMMENTS:

  1. SI! KWASIMBA HII WAJE TENA TUNAWASUBIRIA KWA SHAUKU KUBWA WATATUFUTA MAJONZ YA KUONDOKEWA NA RAIS WETU MTETEZI WA WANYONGE

    ReplyDelete
  2. Coach asiongee sana, wenzake watacheza mpira ndani na nje, sitashangaa nikusikia wachezaji 10 wa AS Vita wanaCorona, ilikuwapunguza nguvu.
    Kwasababu vyovyote iwavyo ushindii inatakiwa CAF inabidi wawemakini na hili suala la upimaji wa Corona, kuna team zinaonewa sana kwa kisingizio cha Corona

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bangi mbaya sana, hivi simba ndio wanapima watu Corona? Hao vita ni bora kuliko ahly? Mbona hakukua na mchezaji wa ahly aliekutwa na corona lkn walifungwa na walizidiwa uwanjani? Halafu tuwafanyie figisu merreikh au vita? Utopolo acheni wivu na chuki zisizo na maana.

      Delete
  3. mbona mwarabu wa misri hajakutwa na korona na amekalia sembuse merekhe nan ukiambiwa wana korona bax ujuwe wanayo mbona kwao walikutwa wa 5 wenye korona hata hao vita wakiwanayo wataambiwa tu

    ReplyDelete
  4. Mkapa stadium the king of jungle a.k.a the lions always win and not be defeated,so get prepared VITA Club

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic