March 17, 2021




NAHODHA wa kikosi cha Tanzania Prisons, Benjamin Asukile amefunguka kuwa uchovu wa kusafiri umbali mrefu baada ya kucheza na Simba, ndiyo sababu kubwa iliyowafanya washindwe kupata ushindi mkubwa zaidi kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania.


Jumapili Prisons iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya kikosi cha JKT Tanzania, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga mkoani Rukwa.

Kabla ya mchezo huo Prisons walikuwa na kibarua kizito dhidi ya Simba kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam Machi 10.

Akizungumzia mchezo huo, Asukile amesema: “Tunashukuru Mungu kwa ushindi tulioupata katika mchezo wetu uliopita dhidi ya JKT Tanzania, ulikuwa mchezo mgumu na nikiri wapinzani wetu walikuwa bora hasa kwenye kipindi cha kwanza.

“Hii yote ilitokana na uchovu ambao tulikuwa nao baada ya kusafiri umbali mrefu baada ya mchezo wa sare dhidi ya Simba, lakini tulijitahidi kupambana na kipindi cha pili tukarejea kwenye kasi yetu ya kawaida, na naamini kama isingekuwa uchovu kikosi kingepata matokeo mazuri zaidi kwenye mchezo wetu” .


5 COMMENTS:

  1. Kuwa wazi bro. Ni uchovu baada ya kutumia nguvu 200% dhidi ya Simba, unasingizia safari Kwan ndo mara ya kwanza mmesafiri

    ReplyDelete
  2. Hayo ndio madhara ya KUKAMIA MECHI, prison amkeni sasa acheni KUCHEZA mpira kwa maelekezo yasiyo rasmi haswa kutoka kwa mashabiki, ukikamia mechi basi jipange kwa mambo kama hayo yanayotokea, kupata matokeo yasiyoridhisha na wachezaji wengi kua na majeruhi ya muda MREFU na uchovu unaosababishwa na kutumia nguvu nyingi. Poleni sana ila hayo tuliyatarajia baada ya mechi.

    ReplyDelete
  3. Mpira kwata pumzi imekata, ha!ha!haaa! Askari wawapi ninyi wachovu Kama utopolo

    ReplyDelete
  4. Kwanza wana chekesha awa mpila kwata alaf mna choka kzembe hvyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic