BENCHI la ufundi la klabu ya Azam kwa kushirikiana na uongozi
wa kikosi hicho, umeamua kuwapa nyota wote wa kikosi hicho mapumziko ya wiki
mbili kupisha ratiba ya michezo ya kimataifa ya kirafiki.
Azam ni miongoni mwa timu ambazo zimefanikiwa kutoa nyota
wengi kutoka kikosi chao cha kwanza, ambao wamekwenda kujiunga na vikosi vya
timu za mataifa yao kwa ajili ya michezo ya kutafuta tiketi ya kufuzu michuano
ya AFCON.
Akizungumzia hilo, Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Azam,
Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ amesema: “Baada ya ligi kusimama kwa muda kupisha
ratiba ya michezo ya kimataifa, benchi la ufundi pamoja na uongozi umeamua
kuwapa mapumziko ya wiki mbili nyota wetu wote.
“Hii inamaanisha wachezaji wetu wote ikiwemo wale ambao hawajaitwa kwenye vikosi vya timu za Taifa, watakuwa na mapumziko ya wiki mbili na watarejea pamoja na wenzao waliojiunga na timu za taifa baada ya muda huo,"







0 COMMENTS:
Post a Comment