March 27, 2021


 UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa bado heshima ya Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli itazidi kuishi kutokana na mambo makubwa ambayo ameyafanya kwa taifa la Tanzania.

Maguli aliyetangulia mbele za haki Machi 17,2021, Machi 26 alipumzishwa kwenye makazi yake ya milele, Chato mkoani Geita katika makaburi ya familia ya Magufuli.

Kuondoka kwake kumeacha simanzi kwenye mioyo ya Watanzania pamoja na Waafrika kwa sababu alikuwa ni mtetezi wa wanyonge, mpenda haki bila kusahau kutekeleza majukumu yake kwa wakati.

Furaha yake kwenye michezo ilikuwa ni kuona timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars inashinda huku kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara maono yake ilikuwa ni kuona kwamba siku moja timu moja inatwaa Kombe la Afrika, (Ligi ya Mabingwa Afrika).

Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit, amesema kuwa Magufuli alikuwa ni kiongozi shujaa na mwenye msimamo katika kusimamia kile anachokiamini.

"Magufuli alikuwa ni kiongozi makini na mwenye msimamo, atakumbukwa kwa kuwa mengi aliyokuwa akiyafanya yanaonekana na yanaleta matokeo kwa kila Mtanzania.

"Ukianza na kuruhusu kuanza kwa michezo mapema kwa timu zote za bara la Afrika haikuwa jambo jepesi ila aliamini inawezekana wakati ule wa janga la Corona.

"Tanzania ilikuwa ni nchi ya kwanza kuruhusu mashabiki kuingia uwanjani na mechi zikaendelea kama kawaida ambapo kuna mataifa mengine yalifuta ligi zao na nyingine zilisismamisha ligi kwa muda mrefu na ziliporudi mashabiki hawakuruhusiwa kuingia," amesema.

1 COMMENTS:

  1. Kwanza kabisa kifo hakichagui wa kumchukuwa wakati ukifika ila kutokana na upambanaji wa kujitoa wa Magufuli katika kutetea maslahi ya Tanzania na Africa kwa ujumla ilikuwa ni vigumu kutabiri kesho ya Magufuli itakuwa vipi kutokana na historia ya wapambanaji halisi wa Africa waliomtangulia waliokuwa wamejitoa muhanga kupigania maslahi ya Africa kufa vifo vya utata au tuwe wazi zaidi kuuliwa.Kuna vitu vitatu ambavyo mabeberu wanatumia kuendelea kuutawala ulimwengu kwa jinsi wanvyotaka wao.Kwanza kabisa hofu.Hofu hiyo iwe kwenye maradhi au nguvu za kijeshi au matatizo ya kisiasa nakadhaika.
    Pili nguvu ya pesa.Haki na watu watanunuliwa hapa kusalitiana wao kwao kusafisha njia ya kupatikana kiongozi kibaraka atakae tetea maslahi ya mabeberu.
    Tatu Media ama propaganda machines.Iwe television, radio, simu nakadhaika.Mababeru wamefanikiwa kwenye hili kwa kiasi kikubwa.Mfano ukiangalia picha za television za ughaibuni utadhani hakuna mtu kufa na kila kitu ni raha ila ukweli sio hivyo kabisa ni kupumbaza watu wa mataifa mengine ili kuwatawala kifikra.Mfano kwa kipindi Cha miaka mitano tu Magufuli amefanya Mambo ambayo Dunia inajiuliza amefanya vipi? Ila wakati huo huo vyombo vyingi vya habari vya kimangharibi vilitumia nguvu kubwa ktangaza machache mabaya ya kubuni ya Magufuli kuiaminisha Dunia kuwa Magufuli ni kiongozi mbaya asiefaa kuwa mfano wa kuigwa Africa ila siku zote ukweli huwa taabu kufichika. Kwa upande wetu watanzania lazima tutubu zambi zetu hasa kwa upande wa upinzani.
    Upinzani Tanzania walimsulubu Magufuli tangu alipoingia madarakani bila kupumzika mpaka wanahakikisha anakufa.Non stop attacks after attack. Lies after lies till he dies.Bila ya kigugumizi nathubutu kusema viongozi wa upinzani hasa wale kutoka chadema na ACT wazalendo hakujawahi kutokea wakati wa furaha katika maisha yao Kama kushuhudia kifo Cha Magufuli akiwa madarakani na kwa kuthibitisha hilo baadhi yao wanasherekea kabisa kwenye mitandao ya kijamii.Ila kama watanzania tunaamini kuwa watu hawa Wana nia njema na nchi yetu basi sisi watanzania ni wapumbavu miongoni mwa wapumbavu wa Dunia.
    Magufuli amekuja kuifumbua macho Africa na Dunia kwa ujumla kuwa kweli Africa sio Masikini.Magufuli amekuja kuthibitisha kuwa muafrica anaweza.Magufuli amekuja kuthibitisha kuwa Africa chini ya muafrica kwa rasimali za Africa inaweza kupata maendeleo tena ya haraka mno.
    Magufuli amekuja kuthibitisha kuwa Vita zidi ya corruption ama ubazirifu na ufisadi Africa inawezekana Magufuli ametujengea hali ya upambanaji na kujiamini watanzania.Wasia wangu ama nasaha kwa watanzania wenzangu tusikubali kurudi nyuma kule kwenye uzembe na uvivu.Tumuenzi Magufuli kwa kudumisha ukakamavu.
    Kwa serikali ya Raisi Samia Suluhu afahamu tu
    kuwa wabaya wa Magufuli bado wapo na ndio wabaya wake yeye pia. Wala asije akapepesuka na hila za watu hao.
    Mama Samia ili afanikiwe na kuwa Mwanamke kiongozi mfano Africa na Duniani lazima asimamie misingi ileile ya Magufuli bila ya kigugumizi la sivyo atachemka. Wakati wa uhai Wake Magufuli kazi kubwa alifanya ya kutafuta viongozi Safi wazalendo wa kufanya nae kazi serikalini.Viongozi hawa Muheshimiwa Raisi Samia anatakiwa kuwaenzi na kuwalea katika Misingi ileile ya Magufuli.
    Muheshimiwa Raisi Samia Suluhu anatakiwa kutotizama nyuma tena kwa maana Kuna viongozi wa serikali ya kikwete akiwamo kikwete mwenyewe wangetamani sasa kutia mkono kwenye uongozi wake.Raisi akikubali hali hiyo itokee basi haitakuwa na mwisho mwema kwenye uongozi wake.Vita zidi ya Rushwa iendelee kwa Kasi zaidi. Ukusanyaji wa mapato usimamiwe kiutaalam zaidi.Na uwajibikaji kusiwe na msalie mtume kwa kiongozi yeyote yule akikiuka maadili ya kazi yake. Mwisho uteuzi wa Makamo wa raisi lazima awe mwanamme wa shoka alieshiba uzalendo.Akiwa kijana kidogo itapendeza zaidi kwani Magufuli aliwahi kutabanaisha hilo Kuwa nchi inapokwendea ni utawala wa vijana.
    wanamichezo tunasikitika kumpoteza kiongozi mashindani wa kweli ila tunakikiwa kuishi na kufanya kazi kwa vitendo kwenye Misingi ya maisha ya Maguful.Mungu aipumzishe roho yake mahala pema.Amin.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic