March 27, 2021


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa suala la ubingwa wa Ligi Kuu Bara pamoja na ule wa Kombe la Shirikisho ni hesabu kubwa kwao na wana amini kwamba watafanikiwa kutwaa taji hilo.

Kwa sasa Yanga inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23 msimu wa 2020/21.

Kwa sasa Yanga ipo chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi ambaye amechukua mikoba ya Cedric Kaze aliyechimbishwa kazi Machi 7 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msola amesema kuwa hakuna sababu ya kuacha kufikiria kutwaa ubingwa kwa sasa kwa kuwa bado kuna mechi za kucheza na ligi inaendelea.

"Ipo wazi kwamba bado kazi ya kusaka ubingwa haijaisha na kila timu ina nafasi ya kutwaa taji hilo kikubwa ni kuona kwamba tunaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea.

"Mashabiki wanahitaji ushindi hata sisi pia tunahitaji kuona hivyo na kwa namna ambavyo tumejipanga bado tuna nafasi ya kutwaa ubingwa.

"Wasiwasi unaonekana kuwepo kwa mashabiki hilo linapaswa liondolewe kwa sasa kwani tayari wachezaji wamejua makosa yao na kutokana na kutokuwa na matokeo mazuri tunahitaji kujenga benchi jipya la ufundi," amesema.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara ni Simba wapo nafasi ya pili na pointi zao ni 46 baada ya kucheza jumla ya mechi 20.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic