UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa unafikiria kurejea kwenye nafasi yao ambayo walianza nayo kwenye mzunguko wa kwanza ambayo ilikuwa ni namba moja kwa kuwa bado wana jambo lao.
Azam FC kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza mechi 24 imekusanya point 44 na kinara ni Yanga mwenye pointi 50 baada ya kucheza mechi 23.
Mzunguko wa kwanza Azam FC ilianza kwa kasi na ilicheza jumla ya mechi 7 bila kupoteza na kufanikiwa kukaa kileleni kwa muda na pointi zao 21 kibindoni zama za kocha Arstica Cioaba ambaye alifutwa kazi kwa kile kilichoelezwa kuwa mwendo wake haukuwa bora.
Kwa sasa kikosi kipo chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina ambaye anaendelea na majukumu ya kuwanoa matajiri hao wa Dar.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kupata matokeo chanya kwenye mechi zao zote ili kurudi kwenye nafasi itakayowafanya waweze kutimiza malengo waliyojiwekea.
"Azam FC tunapenda kuona kwamba kwenye kila mechi tunapata matokeo chanya kwa kuwa malengo ili yatimie ni lazima kupata matokeo hakuna jambo lingine.
"Tunahitaji kuona kwamba baada ya msimu kuisha tunaweza kutimiza jambo letu hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti kila kitu kinawezekana," .
0 COMMENTS:
Post a Comment