March 28, 2021


 UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa imani yao kubwa kwa sasa ni kuweza kurejea kwenye uimara na kupata matokeo chanya katika mechi zao zilizobaki licha ya kuyumba kwa muda.

Machi 7, Yanga walimfuta kazi Cedric Kaze raia wa Burundi na msaidizi wake Nizar Khalfan ambaye ni mzawa kwa kile ambacho walieleza kuwa ni mwendo mbovu wa timu hiyo.

Katika mechi sita, Kaze aliongoza kikosi hicho kushinda mechi moja, sare nne na alipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union ni kwenye mzunguko wa pili.

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa yote ambayo wanapita ni kipindi cha mpito yatakwisha na maisha yataendelea.

“Tukiwa ni timu tunatambua kwamba mashabiki wanahitaji kuona tunapata matokeo hilo ni jambo jema nasi tunalifikiria. Kuyumba ni kwa muda tunaamini kwamba tutarejea kwenye ubora na kila kitu kitakwenda sawa.

“Ni mapema kwa sasa kukata tamaa kwa sababu kuna mechi zipo ambazo tutacheza na tuna amini kwamba wachezaji wetu ni wazuri na watapambana kupata matokeo," .

Yanga ipo mikononi mwa Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi ambaye ameanza mazoezi na kikosi kambini Kigamboni.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza na imekusanya jumla ya pointi 50 baada ya kucheza mechi 23.

Miongoni mwa wachezaji ambao wameanza mazoezi ni pamoja na Paul Godfrey, 'Boxer', Ramadhan Kabwili, Faroukh Shikhalo, Michael Sarpong.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic