March 3, 2021


 BAADA ya beki wa kushoto ndani ya kikosi cha Azam FC, Bruce Kangwa kuongeza dili la mwaka mmoja ndani ya timu hyo amesema kuwa leo wamekubaliana kupambana kusaka pointi tatu ndani ya uwanja.

Machi Mosi, Kangwa ambaye mkataba wake ulikuwa unamalizika Agosti 2021, aliongeza dili jingine hivyo bado yupo ndani ya kikosi hicho mpaka msimu wa 2022.

Leo kikosi cha Azam FC chini ya George Lwandamina ambaye ni Kocha Mkuu, kina kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba na utakuwa ni mchezo wake wa kwanza baada ya kusaini dili hilo jipya.

Kangwa amesema:-"Wachezaji tumekubaliana kwamba lazima tupambane ndani ya uwanja kupata pointi tatu muhimu hakuna jambo nzuri kama kushinda hivyo tupo tayari katika hilo.

"Ipo wazi kwamba mchezo utakuwa mgumu kwani kwa sasa ligi imekuwa na ushindani mkubwa hilo tunalitambua hivyo tunaingua ndani ya uwanja kwa nidhamu na tahadhari ila lengo ni pointi tatu,"

Mchezo wa kwanza walipokutana zama za Arstica Cioaba, Azam FC ilishinda mabao 4-2, Uwanja wa Azam Complex.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic