March 31, 2021


ALMAS Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania,(TPLB) amesema kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea Aprili 8 baada ya kutimiza siku 21 za maombolezo.

Ligi ilisimama kwa muda kutokana na msiba wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Joseph Magufuli ambapo zilitolewa siku 21 za maombolezo.

Magufuli alitangulia mbele za haki Machi 17 jambo lilipolekea Serikali kutoa siku 21 za maombolezo ambazo bado zinaendelea kwa sasa.

Kasongo amesema:- "Ukitazama ratiba yetu ile ya awali ambayo tuliitoa kwa vilabu ilikuwa inaonyesha kwamba tarehe 3-4 Machi, michezo ya Kombe la Shirikisho, tarehe 6-8 Machi tulikuwa tunarejea kwenye mechi za ligi.

"Kutokana na msiba tafsiri yake ni kwamba ile michezo ya Shirikisho na ile ya ligi nayo inakuwa haipo kwa sababu tupo kwenye maombolezo ya siku 21.

"Kumbuka kwamba siku 21 zinaisha tarehe 7 ambapo kulikuwa na mchezo wa ligi, tarehe 6 kulikuwa na mchezo wa ligi na tarehe 3-4 kulikuwa na mchezo wa Kombe la Shirikisho.

"Baada ya kuipitia ratiba yetu tumekuja na mabadiliko. Unaweza kuona kwamba ligi yetu inarejea tarehe 8, 9 na 10 Aprili, michezo ya tarehe 6 na 7 itachezwa tarehe 9-10 michezo iliyopaswa kuchezwa tarehe 10 ipo palepale.

"Ligi yetu itaendelea tarehe 8, 9 na 10 itakuwa michezo ya awali ya kufungua ligi yetu kutoka pale ambapo tulisimama kwa siku 21 za maombolezo.

"Kuna baadhi ya michezo imeweza kufa inabidi itafutiwe siku nyingine na kuna michezo mingine ya kiporo nayo itatafutiwa siku," .


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic