March 23, 2021


NYOTA wa Simba, Clatous Chama amewaambia mabosi wake kuwa kaka yake Adrian Chama ana uwezo mkubwa uwanjani kumshinda yeye hivyo wakimpa mkataba atafurahi kucheza naye.

Chama ana miaka 29 kaka yake Chama anayecheza ZESCO United ana miaka 32 na wote wamekuwa wakipata nafasi ya kucheza timu ya Taifa ya Zambia.

Kaka yake Chama, nafasi yake uwanjani ni beki huku mdogo wake Chama anacheza nafasi ya kiungo yupo zake pia timu ya Taifa ya Zambia.

Chama amesema:"Ninajua kwamba kaka yangu ana uwezo mkubwa na anajua mpira hivyo akipata nafasi ya kucheza Simba atafanya vizuri na kuleta changamoto kwa wengine.

"Ninamjua na ninapenda kuwa naye kila mahali hivyo hakuna tatizo ikiwa Simba watamsajili watakuwa wamepata mchezaji mzuri,".

Simba kwa sasa inashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa imetinga hatua ya makundi ampapo ikiwa kundi A inaongoza kundi hilo na pointi zake ni 10.

Inafuatiwa na vigogo Al Ahly ambao wapo nafasi ya pili na pointi zao ni 7. Mechi yao ijayo ni dhidi ya AS Vita ambayo ipo nafasi ya tatu na pointi 4.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic