March 4, 2021


 MSHAMBULIAJI wa Yanga Ditram Nchimbi ni miongoni mwa nyota ambao wataukosa mchezo wa leo, Uwanja wa Mkwakwani dhidi ya Coastal Union. 


Kwa mujibu wa Kocha Mkuu, Cedric Kaze amesema kuwa Nchimbi ambaye jina lake lipo kwenye orodha ya nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania,  Taifa Stars aliumia Kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Ken Gold. 


Mbali na Nchimbi mwenye pasi mbili za mabao kati ya 34 yaliyofungwa na Yanga pia Adeyum Saleh yupo kwenye orodha hiyo baada ya kuumia kwenye mazoezi ya mwisho.


Saido Ntibanzokiza na Balama Mapinduzi hawa bado hawajarejea Kwenye ubora huku Carlos Carlinhos kadi nyekundu aliyopata mbele ya Ken Gold ikimuweka nje.


Mchezo huo wa Ligi Kuu Bara ambao ni mzunguko wa pili utachezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.


Mchezo wa kwanza, Yanga ilishinda mabao 3-0, Uwanja wa Mkapa hivyo leo itakuwa ndani ya Mkwakwani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic