March 29, 2021


 BAADA ya Cedric Kaze aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga, kufutwa kazi Machi 7 kwa kile kilichoelezwa kuwa ni matokeo mabovu, Mfaransa Sebastian Migne anatajwa kuwasili Bongo kuchukua mikoba yake.


Kaze alitoa Bongo kuchukua mikoba ya Zlatko Krmpotic ambaye alifutwa kazi baada ya kuongoza mechi tano za Ligi Kuu Bara,  alishinda nne na sare ya kufungana bao 1-1 na Tanzania Prisons,  Uwanja wa Mkapa.


Kaze raia wa Burundi, mzunguko wa pili mambo yalikuwa magumu kwake ambapo katika mechi 6, alishinda moja, sare nne na alipoteza kwa kufungwa mabao 2-1 mbele ya Coastal Union,  Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Raia huyo wa Burundi alitua Bongo, Oktoba 15,2020 na mchezo wake wa kwanza ilikuwa Uwanja wa Uhuru dhidi ya Polisi Tanzania timu yake ikishinda bao 1-0 na mchezo wake wa mwisho ilikuwa dhidi ya Polisi Tanzania, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, alishuhudia ubao ukisoma Polisi Tanzania 1-1 Yanga.

Wakati anachimbishwa ndani ya kikosi hicho ambacho kwa sasa kipo mikononi mwa Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi, kikosi kwenye msimamo kina pointi 50 na kipo nafasi ya kwanza.

Mchakato mzima wa kumsaka mbadala wake ulianza mara moja siku aliyofutwa kazi yeye na benchi lake la ufundi ambapo msaidizi wake pia Nizar Khalfan ambaye ni mzawa naye alifutwa.

Kwa mujibu wa Dominic Albinius, Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi wa Yanga amesema kuwa mchakato unakwenda vizuri na wanaamini watapata kocha makini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic