March 29, 2021

 


GANZI kubwa kwa timu ambazo zinashindwa kupata matokeo uwanjani zinatokana na ushindani ambao upo kwa msimu wa 2020/21 jambo linalofanya kila timu kupambana kupata matokeo.

Katika matokeo kumekuwa na rekodi ambazo zinawekwa na timu pamoja na wachezaji wenyewe uwanjani. Hapa tunakuletea namba ndani ya ligi namna hii:-

206

Jumla ya mechi za ligi ambazo zimechezwa mpaka sasa kwenye ardhi ya Bongo.

50

Pointi za vinara wa ligi Bongo ambao ni Yanga wakiwa wamecheza jumla ya mechi 23 na kujikusanyia pointi 50 msimu wa 2020/21.


Wamepoteza mchezo mmoja ilikuwa Uwanja wa Mkwakwani, ubao ulisoma Coastal Union 2-1 Yanga.

46

Idadi ya vinara wa mabao ndani ya ligi ambao ni Simba. Wamefunga mabao hayo baada ya kucheza jumla ya mechi 20.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya pili na imekusanya pointi 46.

John Bocco na Meddie Kagere wanaongoza orodha ya wafungaji wenye mabao mengi wapo ndani ya Simba kila mmoja ana mabao 9.

44

Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina imekusanya pointi 44 baada ya kucheza mechi 24.

43

Timu ya Mwadui FC ya Shinyanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Amri Said imebebeshwa zigo la mabao 43. Ni namba moja kwa timu zilizokusanya mabao mengi.

Imecheza mechi 24 imekusanya pointi 16 na imefunga mabao 17 ipo nafasi ya 18.

Inaongoza pia kwa timu iliyopoteza mechi nyingi ambazo ni 16 imeshinda mechi nne.

18

Namungo FC ya Hemed Seleman, ‘Morocco’ imecheza mechi chache kuliko timu nyingine. Ni mechi 18 kwa inafuatiwa na Simba ambayo imecheza mechi 20.

 Timu hizi mbili zinawakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa.

Namungo ikiwa nafasi ya 10 na pointi 27 ipo kwenye Kombe la Shirikisho na Simba ipo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika zote zipo hatua ya makundi.

11

Polisi Tanzania ya Malale Hamsini  imekusanya sare 11 kwenye ligi. Ni namba moja kwa timu zenye sare nyingi. Ina pointi 29 ikiwa ipo nafasi ya 8.

9

Mtibwa Sugar safu yake ya ushambuliaji imefunga jumla ya mabao 9 ikiwa imecheza mechi 22. Safu ya ulinzi imeokota mabao 16.

Mtibwa Sugar imekwenda tofauti na Simba ambayo imefungwa mabao 9 kwenye mechi zake 20 ambazo imecheza.

6

Timu 7 ndani ya ligi zimeshinda jumla ya mechi 6. Timu hizo ni :-Polisi Tanzania, Prisons, Coastal Union, Gwambina, Kagera Sugar, JKT Tanzania, Mtibwa Sugar.

4

Timu ambazo zitashuka daraja msimu huu wa 2020/21 na zitashiriki Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2021/22. Ni zile zitakazomaliza ligi kuanzia nafasi ya 15-18

3

Mbeya City imeshinda mechi chache ambazo ni tatu kati ya 23 ambazo imecheza. Ina pointi 20, imekusanya sare 11, poteza 9.

2

Itashuhudiwa mechi mbili za playoff kwa timu za mbili zinazoshiriki ligi na mbili za Ligi Daraja la Kwanza, mshindi wa jumla atashiriki ligi msimu ujao.

Kutoka ndani ya ligi ni zile zitakazokuwa nafasi ya 13-14 na kwa upande wa Ligi Daraja la Kwanza zile ambazo zitakuwa nafasi ya pili kwenye makundi mawili ambayo ni A na B.

Makala kutoka dawati la Spoti Xtra.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic