KESHO Machi 6, kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kina kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Al Merrikh kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Gomes ana kazi ya kusaka pointi tatu ili kuweza kuitafuta nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali kwa kuwa ana pointi sita ikitokea akashinda atafikisha pointi 9.
Ana kibarua kizito mbele ya timu hiyo ambayo haijaambulia ushindi kwenye mechi zote mbili ambazo amecheza ndani ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kiungo wake Luis amekuwa gumzo Afrika kutokana na wezo wake anaounyesha ndani ya uwanja kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.
Hiki hapa kikosi cha kwanza ambacho kinatarajiwa kuanza mbele ya Al Merrikh:- Aishi Manula
Shomari Kapombe.
Pascal Wawa.
Joash Onyango.
Mohamed Hussein,'Tshablala'.
Luis Miquissone.
Mzamiru Yassin.
Thadeo Lwanga.
Rarry Bwalya.
Clatous Chama.
Chris Mugalu.
Haya
ReplyDeleteKesho Nyoni ataanza pamoja na lwanga
ReplyDeleteHawa ni wachezaji wawili ambao chemistry yao haijaendana. Hawawezi kuanza pamoja
DeleteKikosi cha otometiki hicho
ReplyDeleteKesho tena mtoe kikosi kingine kinachotarajiwa
ReplyDelete