March 5, 2021

 
 


KIUNGO mshambuliaji wa Yanga, Balama Mapinduzi ‘Kipenseli’, unaambiwa amepata nafuu ya majeraha yake na hivi karibuni anatarajiwa kuanza mazoezi mepesi.


Kiungo huyo ataanza mazoezi baada ya kupata nafuu ya majeraha ya kifundo cha mguu aliyoyapata akiwa mazoezini kabla ya hivi karibuni kusafirishwa kwenda Afrika Kusini kwa ajili ya kufanyiwa upasuaji.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli alisema kuwa kiungo huyo anaendelea vizuri na ataanza mazoezi mwanzoni mwa mwezi huu.

 

Bumbuli alisema kiungo huyo ataanza mazoezi akiwa chini ya uangalizi wa madaktari wa timu hiyo ili kuhakikisha anapona kabisa.

 

“Taarifa njema kwa mashabiki wote wa Yanga, kuwa kiungo wao kipenzi Mapinduzi amepata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji. “Na mwanzoni mwa mwezi huu Machi, mwaka huu ataanza programu za mazoezi mepesi chini ya uangalizi wa madakatari wa timu,” alisema Bumbuli.

STORI NA WILBERT MOLANDI, Dar es Salaam

1 COMMENTS:

  1. Too late, when others start, Simba is already approaching the horison with supersonic speed

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic