ROY Keane, mchezaji wa zamani wa Klabu ya Manchester United mwenye umri wa miaka 49 amesema kuwa ili Harry Kane nyota wa Klabu ya Tottenham Hotspur apate mafanikio zaidi ni lazima ahame hapo alipo.
Mbali na Keane pia Ashley Cole mwenye miaka 40 mchezaji wa zamani wa Klabu ya Chelsea na Arsenal amesisitiza jambo hilo kwa Kane.
Mkataba wa Kane mwenye miaka 27 ndani ya Klabu ya Tottenham Hotspur inayonolewa na Jose Mourinho unatarajiwa kumeguka 2024 ila inaelezwa kuwa zipo timu ambazo zinampigia hesabu.
Manchester City na Manchester United inaelezwa kuwa zinahitaji saini ya mshambuliaji huyo ambaye yupo pia ndani ya timu ya Taifa ya England na alifunga bao moja dakika ya 38 wakati timu yake ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Albania mchezo wa kuwania kufuzu Kombe la Dunia.
Cole amesema kuwa kila siku amekuwa akimsikia nyota huyo akizungumzia kuhusu timu yake kwamba anafuraha jambo ambalo linanishangaza.
"Muda mwingi nimekuwa nikimsikia Kane akisema kuhusu Spurs kuwa anafuraha na anapenda kuwa hapo. Sawa ila jambo la kujiuliza anaweza kushinda ama anataka kuwa hivyo alivyo?
"Ikiwa anahitaji kushinda zaidi tuzo basi anastahili kufikiria kuhama hapo kupata changamoto mpya, itakuwa vizuri kwake lakini anapaswa kufikiria mafanikio yake.
"Yeye ni mchezaji mkubwa anapaswa kuwa katika timu kubwa na ni lazima mchezaji mkubwa ashinde mataji pamoja na tuzo binafsi, sina uhakika kama timu yake inaweza kumaliza ndani ya nne bora," .
0 COMMENTS:
Post a Comment