MBWANA Samatta, nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa haikuwa hesabu zao kuishia hatua ya makundi katika kuwania kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika,(Afcon).
Stars ilimaliza mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi jana Machi 28 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Libya, Uwanja wa Mkapa.
Ushindi huo wa Stars umewanyima fursa ya kushiriki Afcon nchini Cameroon kutoka kundi J ambalo Tunisia ni vinara na pointi 16 wakifuatiwa na Equatorial Guinea wenye 9 na Libya nafasi ya nne na pointi 3.
Ikiwa na pointi zake 7 nafasi ya tatu ina kazi ya kujipanga upya kwa ajili ya wakati ujao kufanya vizuri hasa katika mechi za mwanzo ambazo imekuwa ikipata tabu kupata matokeo.
Samatta amesema:"Haikuwa malengo yetu kuishia hapa tunajua mashabiki wameumia, hata sisi tumeumia tutajipanga upya wakati ujao,".
0 COMMENTS:
Post a Comment