March 20, 2021


 


KOCHA mkuu wa AS Vita, Florent Ibenge amesema kuwa ili waweze kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Afrika wanatakiwa kuibuka na ushindi katika michezo yao miwili iliyosalia ya ligi hiyo ikiwemo dhidi ya Simba.

AS Vita kwa sasa inashika nafasi ya 3 katika kundi A la ligi ya mabingwa mara baada ya kujikusanyia pointi 4 nyuma ya Simba waliona pointi 10 na Al Ahly ambao wamejikusanyia pointi saba.

Akizungumzia malengo yao katika michuano hiyo Ibenge amesema: “Tunatakiwa kushinda michezo yetu yote miwili iliyosalia dhidi ya Simba na Al Merrikh ili tuweze kusonga mbele katika hatua ya robo fainali.

"Matokeo tuliyopata hayajakuwa mazuri sana kwetu, lakini huu si muda wa kulaumiana tunachotakiwa kufanya ni kuhakikisha tunasonga mbele.

AS Vita wanatarajia kucheza na Simba ugenini Aprili 2, katika Uwanja wa Mkapa, Dares Salaam huku mchezo wa mwisho ukitarajiwa kufanyika kwao nchini Congo April 9, wakicheza dhidi ya Al Merrikh.

 

 

 

 

 

 

 

7 COMMENTS:

  1. Aje tu tunahasira zilizojaa majonzi tunahitaji kitu Cha kutuliwaza kwa gharama yeyote ile.

    ReplyDelete
  2. kwa mkapa hatoki MTU,vita watachinjwa mapemaaaa,simba nguvu mojaaa

    ReplyDelete
  3. kwa mkapa hatoki MTU,vita watachinjwa mapemaaaa,simba nguvu mojaaa

    ReplyDelete
  4. No free lunch at benjamin mkapa stadium

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic