March 20, 2021

 


MIAMBA ya soka kutokea nchini Afrika Kusini, Kaizer Chiefs wameonyesha nia ya kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Nigeria, Junior Lokosa, ambapo inaelezwa Simba wanahitaji dau la dola 200,000 sawa na zaidi ya Shilingi Milioni 464.

Lokosa alijiunga na Simba kwenye dirisha la usajili la mwezi Januari, lakini tangu atue ndani ya kikosi cha timu hiyo ameonekana kupata wakati mgumu kuingia kwenye kikosi cha kwanza cha Simba, mbele ya Chris Mugalu ambaye ndiye chaguo la kwanza la kocha, Didier Gomes.

Inaelezwa kuwa kikosi cha Strømsgodset Toppfotball ya nchini Norway, kilichoonyesha nia ya kumuhitaji nyota huyo kimejiondoa kwenye mpango huo.

Akizungumzia ofa hiyo ya Kaizer Chief, Katibu Mkuu wa Simba, Dk Arnold Kashembe amesema: “Sijapokea taarifa zozote kuhusiana na ofa ya klabu ya Kaizer Chief kumtaka mshambuliaji wetu, Junior Lokosa.

“Hivyo siwezi kusema lolote kwa sasa lakini iwapo kutakuwa na taarifa yoyote rasmi kuhusiana na hilo basi tutawaeleza,”

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic